Menu
STARS Project
close
STARS Project
close

Refine your search

STARS Project
Kutuhusu


STARS ni mradi wa utafiti unaotafuta namna ya kutumia teknolojia ya utambuzi kwa njia ya satelaiti ili kuboresha shughuli za kilimo katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini. Mradi huu unafadhiliwa na Bill & Melinda Gates Foundation. Mradi una lengo la kuboresha maisha ya wakulima wadogo wadogo katika maeneo hayo.


Utangulizi – Changamoto

Hivi karibuni Nchi zenye vipato vikubwa duniani zimeboresha mfumo wa usimamizi wa kilimo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kukusanya taarifa kwa njia ya picha za satelaiti na ndege zisizotumia rubani. Mbali na taarifa zinazokusanywa, ushauri unaweza kutolewa kwa wakulima mashambani kusaidia kufanya maamuzi yao kuhusu mbinu za kilimo. Hii inasaidia upatikanaji wa mazao bora na uzalishaji endelevu. Taarifa hizi pia zinaweza kusaidia maamuzi ya ngazi za juu serikalini katika kusimamia usambazaji wa chakula kitaifa wakati wa ukame kwa usahihi zaidi.

Uhalisia wa kilimo katika katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini umesababisha ugumu wa matumizi ya teknolojia ya picha za satelaiti. Kwa mfano, wakulima wadogo, ambao huzalisha theluthi mbili ya chakula duniani, mara nyingi wana mashamba madogo madogo na mipaka iliyo pinda pinda na alama za kienyeji za sehemu husika. Pia wakati wa msimu hupanda mazao ya aina nyingi mchanganyiko na kwa tarehe tofauti kwenye shamba moja na hakuna vigezo maalum vya matumizi ya mashamba hayo. Hali hii inasababisha ugumu wa kutumia taarifa za picha za satelaiti kutofautisha aina ya mazao yaliyopo shambani na hivyo kushindwa kupata kwa usahihi taarifa za maendeleo ya mazao shambani na matarajio ya mavuno ambazo ni muhimu kwa wadau mbalimbali kama wakulima, wafanyabiashara na serikali.


Changamoto nyingi zikiwamo udongo usio na rutuba, magonjwa ya mimea, wadudu na ukame husababisha wakulima wengi kuhangaika katika kuzalisha mazao kiuendelevu mwaka hadi mwaka. Katika ngazi ya kitaifa, changamoto hizi zaweza kusababisha ugumu katika kuelewa hali ya mazao na malisho, matarajio ya hali ya chakula, uhakika wa masoko na kiwango cha uzalishaji katika msimu husika. Maamuzi iwapo chakula cha ziada kinahitajika kuagizwa toka nchi nyinginezo kukabiliana na upungufu katika msimu husika yamekuwa yakifanywa bila kuwa na takwimu za kutosha juu ya mwenendo wa msimu na hali ya mazao shambani. Kumekuwepo mifano pia ambapo chakula kimeagizwa toka nchi za nje wakati ambapo kuna chakula cha kutosha nchini, hali ambayo ilisababisha kuwepo chakula kingi na kusababisha matatizo ya kifedha kwa wakulima wadogo kutokana na kuanguka kwa bei za mazao yao.