Menu
STARS Project
close
STARS Project
close

Refine your search

STARS Project
Kutuhusu

Faida

Kwa njia za kutumia picha za satelaiti na ndege zisizo na rubani tunaweza kutambua kikamilifu, kilimo kusini mwa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini. Teknolojia hii itakuwa na manufaa katika nyanja mbalimbali:

  • Wakulima wadogo wanaweza kupata tathmini ya hali ya mazao yakiwa shambani, kupata ushauri bora wa kuwawezesha kufanya maamuzi bora na endelevu zaidi juu ya aina ya mazao wanayolima, wakati wa kuyapanda, na utunzaji wake. Hii inaweza kusababisha mavuno bora, ubora wa juu wa uzalishaji, kuongezeka utajiri na kuboresha maisha kwa baadhi ya jamii maskini zaidi duniani. 
  • Taarifa sahihi na za uwazi zaidi kuhusu mazao na hali ya mashamba kutawezesha wakulima wadogo na jamii zao kupata haki ya matumizi ya ardhi. Mara nyingi haki ya umiliki wa ardhi husababisha migogoro na wakulima wadogo wadogo kuporwa ardhi zao. 
  • Kwenye mradi wa STARS mkulima hachangii gharama yoyote ile, pia mradi una lengo la kutoa elimu na mafunzo ya kuwezesha taarifa hii ya bure itumike kwa ufanisi zaidi. Zaidi ya hayo, watajaribu kujenga njia ya kuleta maendeleo zaidi na uwekezaji katika teknolojia ya picha za satelaiti na ndege zisizo na rubani kwa ajili ya utambuzi wa kilimo kwa nchi zinazoendelea. 
  • Nchi zinazoibukia kiuchumi zitaweza, kwa uhakika zaidi, kutabiri mavuno katika ngazi ya kitaifa ili kufanya maamuzi thabiti kuhusu hali ya chakula kwa watu wake. 
  • Michakato ya uzalishaji wa chakula katika nchi zinazoibukia kiuchumi utaweza kuwa wa uhakika zaidi kwana masoko ya ndani yataimarika endapo wakulima wataweza kuzalisha kwa ufanisi. Fursa nzuri za kuuza mazao nje zaweza pia kutokeza kutokana na njia endelevu za kilimo, kuweza kuchangia katika uchumi imara zaidi.

Shauku ya STARS ni kujua kama teknolojia ya utambuzi kwa teknolojia ya satelaiti inaweza fanikiwa na kuleta faida. Ni mategemeo ya mradi kwamba teknolojia itaongeza ubora na wingi wa mazao. Pia itasaidia wadau kuwa na uelewa wa uzalishaji wa mazao ya chakula katika nchi zinazoibukia kiuchumi na kuboresha shughuli za kilimo na maisha ya watu kwa baadhi ya jamii maskini zaidi.