Menu
STARS Project
close
STARS Project
close

Refine your search

STARS Project
Kutuhusu

Mradi wa STARS

Kuanzia tarehe 1 Juni 2014, STARS ilianzishwa ili kutafuta mbinu za kutatua baadhi ya changamoto zilizoonekana. Chuo Kikuu cha Twente nchini Uholanzi kinaongoza muungano wa nchi zilizo mbele katika matumizi ya teknolojia ya rimoti katika kilimo duniani. Muungano huu utatafiti baadhi ya fikira kuhusu uhalisia wa taarifa zinazochukuliwa kwa njia ya rimoti na kutathmini aina ya taarifa zenye manufaa zaidi kwa wakulima katika kipindi cha miezi 20 ya mradi. Muungano unajumuisha kundi la kimataifa la taasisi za utafiti, ikiwa ni pamoja na:

  • Shirika la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Umoja wa Madola  (CSIRO) la nchini Australia;
  • Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mazao katika Maeneo Kame ya Tropiki (ICRISAT) zilizo Mali na Nigeria; 
  • Chuo Kikuu cha Maryland cha Marekani kwa kushirikiana na nchi za Tanzania na Uganda; 
  • Kituo cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT) katika nchi za Bangladesh na Mexico.