Menu
STARS Project
close
STARS Project
close

Refine your search

STARS Project
Kutuhusu

Ripoti fupi

Mradi wa STARS tayari unafanya majaribio katika maeneo matatu:

  1. Afrika Magharibi: Mradi una tafiti kuhusu  umiliki wa ardhi katika jamii zaidi ya 20, na mashamba ya wakulima wadogo wadogo binafsi 150 katika nchi za Mali na Nigeria, kudurusu mbinu zitakazotokeza huduma za ushauri rafiki kwa wakulima wadogo wadogo.
  2. Afrika Mashariki: Mradi una tekelezwa katika nchi za Tanzania na Uganda. Lengo kuu ni kufuatilia hatua za ukuaji wa mazao kuanzia kupanda hadi kuvuna katika mashamba tofauti tofauti ya mazao ya chakula ili kupeleka taarifa kwenye Idara ya Usalama wa Chakula na kusaidia kufuatilia hali ya mazao.
  3. Asia Kusini: Mradi mwingine unahusu matumizi ya picha za satelaiti na ndege zisizo na rubani upo nchi ya Bangladesh, Asia ya Kusini. Lengo la mradi ni kusaidia kutathmini mafuriko ya Delta ya Bengal na namna yanavyoweza kutumiwa na wakulima kuzalisha mazao kwa kutumia maji yaliyo juu ya ardhi kulima wakati wa kiangazi.


Pamoja na majaribio mbalimbali kikanda yanayofanyika, fursa hii ya utafiti imelenga kwenye utimiaji wa mifumo ya taarifa za kilimo ambapo teknolojia ya sateliti kuweza kufanya mabadiliko kwenye kilimo. Hii itatoa mwelekeo kuonesha maeneo muhimu ya uwekezeji na njia ya kufanya hivyo. Pamoja na kuwepo kwa majaribio ya kikanda, mradi huu unaangalia kwa mapana zaidi ushirikishwaji kikamilifu wa wadau na mchango unaoweza kutokana na  teknolojia.